Dkt. Abbasi: Hatujaagizwa Kufungulia Magazeti

Magazeti

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee, na siyo pamoja magazeti.

 

 

Dkt. Abbasi amesema hayo leo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais Samia kueleza kuwa vyombo vya habari vilivyofungiwa akitaja Televisheni za mtandaoni zifunguliwe. Dkt. Abbasi amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.

 

 

“Hatujaagizwa na Mhe. Rais @samia_suluhu_hassan tuyafungulie Magazeti tuliyoyafungia, ni Online TV tu tunazifungulia….” Dkt. Hassan Abas, Katibu Mkuu wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Toa comment