The House of Favourite Newspapers

Dkt. Bashiru Alivyomkaribisha Rais Shein Amtambulishe Mgombea wa Zbar

0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru akielezea sifa za mgombea Uraisi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi na kumuomba Rais aliyeko madarakani Dkt. aende kumkaribisha.

Katika shamrashamra za uzinduzi wa kampeni zilizofanyika jana Jijini Dodoma, kabla ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally alitumia nafasi hiyo kumkaribisha Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Shein ili amtambulishe mrithi wake Dkt. Hussein Mwinyi.

Dkt. Bashiru kabla ya  mgombea huyo kupanda jukwaani alimuelezea sifa zake ikiwemo kuzimudu vyema wizara alizowahi kuziongoza ikiwemo wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii pamoja na Wizara ya Ulinzi aliyokaa miaka kumi sasa.

Akielezea fani yake Dkt. Bashiru alisema mgombea huyo taaluma yake ni udaktari wa maradhi ya ndani ya mwili wa binadamu.

Raisi wa Zanzibar Dkt. Shein akiwaomba Wazanzibari kumchagua Dkt. Hussein Mwinyi na kuwaeleza sababu inayomfanya aweze kuwa raisi wao.

Leave A Reply