The House of Favourite Newspapers

Dkt Cheni Afunguka Alivyochaguliwa na Rais wa Zanzibar Kusherehesha Harusi ya Mtoto Wao – Video

MSHEREHESHAJI maarufu nchini na Staa wa filamu, Dkt Cheni.

MSHEREHESHAJI maarufu nchini na Staa wa filamu, Dkt Cheni amefunguka alivyochaguliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na mkewe kusherehesha harusi ya mtoto wao iliyofanyika hivi karibuni Visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi wakubwa akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Viongozi wengine.

Dkt. Cheni amesema haikuwa rahisi wala bahati bali jina lake lilipita mapema na aliyemchagua ni Rais Dkt. Mwinyi kitu ambacho anashukuru sana kwa heshima hiyo.

Licha ya ukubwa wa shughuli na uwepo wa Viongozi wakubwa Dkt. Cheni amesema haikufanya kazi yake iwe ngumu bali alifuata taratibu alizopewa na yeye akaendelea na kazi yake vizuri bila shida yoyote

Hii sio mara ya kwanza kufanya shughuli yenye Viongozi wakubwa bali alishawahi kufanya za Viongozi wengine kama Dkt. Kikwete, Mkapa na hata Watu maarufu kama Wasanii na Mabilionea kitu kilichomjengea uzoefu.

PESA NDEFU ALIYOLIPWA DR CHENI HARUSI ya MTOTO wa RAIS MWINYI – “WATOTO wa BAKHRESSA WALIKUWEPO”…