Dkt. Mwigulu Akagua Miradi ya Kimkakati ya Bandari na Barabara Lindi

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba Desemba 19, 2025 amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya Kikazi.
Dkt. Mwigulu anategemea kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Madaraja na Ukarabati wa barabara Kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo.


