Dkt. Nchimbi Aelekeza Mawaziri wa Viwanda na Kilimo, Kutafutia Ufumbuzi Soko la Korosho



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amepokelewa Mkoa wa Lindi kwa vifijo na nderemo akitokea Mkoani Mtwara akiwa Mnazi mmoja ambapo amezungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wakimsubiri.
Balozi Nchimbi akijibu kero za wananchi wa Mkoa wa Lindi amesema hatutapata mafanikio ya kweli kama tutaendelea kuuza korosho ghafi lazima tubangue wenyewe ili tupate faida sasa natoa maelekezo kwa Mawaziri wa kilimo na Viwanda na Uwekezaji kuhakikisha Korosho yote ibanguliwe hapa hapa nchini ili kuongeza thamani ya zao letu hili na kama viwanda vijengwe ili kukuza uchumi wetu.
Katika ziara hii Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.