The House of Favourite Newspapers

Dkt. Nchimbi Apokea Risala ya Wajumbe wa NEC, Waunga Maazimio ya Mkutano Mkuu CCM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi jana tarehe 27 Januari 2025, amepokea risala ya waliowahi kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), iliyosomwa na Mhandisi Burton Kyaka, wakiunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, ambao ulikutana hivi karibuni jijini Dodoma na kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya CCM, na kumthibitisha Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea pekee wa CCM kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.