Dkt. Nchimbi Ashiriki Uzinduzi wa Treni ya Umeme (SGR) – Video
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akishiriki ratiba mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mradi wa kimkakati wa treni ya umeme (SGR), kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma, kupitia Morogoro, uliofanywa na Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, leo Alhamis, Agosti 1, 2024.
Shughuli ya uzinduzi rasmi ilihusisha pia Mgeni Rasmi Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika vituo vya treni hiyo kumlaki na kumsikiliza wakati akisafiri na treni hiyo kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma.