The House of Favourite Newspapers

DKT SHEIN AHIMIZA WANAFUNZI KUKAZANIA MASOMO

0
Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein akisaini kitabu cha wageni katika shule yaKihinani.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud akiongea na Dkt. Shein.
Wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wakimsikiliza Rais Shein (hayupo pichani).
Msafara wa Rais Shein ukielekea kufungua tawi la CCM la Bumbwisudi.
Wana-CCM wakimsikiliza Rais Shein kabla ya kuzindua tawi lao.
Uzinduzi wa tawi hilo ukiendelea.

 

WANAFUNZI Zanzibar wametakiwa kukazania masomo kwa ajili ya kujijenga maisha ya baadaye badala ya kufanya mambo yasiyoendana na umri na mila zao.

Hayo yalisema na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein, wakati wa ziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Kihinani.

Dkt Shein alikuwa akiweka jiwe la  msingi katika shule hiyo iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi
A iliyojengwa kwa ushirikiano wa wananchi waliochanga shilingi  milioni 24 na serikali ikaongeza nguvu ya shilingi mil.
21.
“Elimu ni nyenzo kubwa sana, iwe elimu dunia au elimu  ahera, na ndiyo maana nikaruhusu elimu bila malipo,
vijana someni msicheze, someni msihadaike kwani mambo mengine wakati wake nyie bado,” alisema Dkt Shein.

Baadaye akiwa Bumbwisudi alikagua mradi wa visima vya maji safi na salama vyenye uwezo wa kutoa maji  zaidi ya lita 220,000 kwa saa na alihitimisha ziara yake kwa leo sehemu hiyo kwa kuweka jiwe la msingi  katika tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) lililopo katika kata hiyo.
Kiongozi huyo anatarajia kuhitimisha ziara yake kesho saa 12 jioni katika Wilaya ya Mjini Magharibi B.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply