Dkt. Slaa Akosa Dhamana, Kuendelea Kusota Rumande Hadi Januari 23
Kesi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwanasiasa mkongwe, Dkt. Wilbroad Slaa (76) ataendelea kusalia kukaa Mahabusu kwa kukosa dhamana baada ya hii leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam kuahirisha Kesi yake ya kusambaza taarifa za Uongo kupitia mtandao wa X hadi Januari 23.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili, Peter Madeleka amesema kuwa kutokana na mwenendo wa shauri hilo kuwa wa chini sasa wameamua kulipeleka shauri hilo mahakama kuu ifikapo Jumatatu ili mteja wao aweze kupatiwa dhamana.