The House of Favourite Newspapers

Dkt. Slaa Atinga Maadhimisho ya Bawacha Siku ya Wanawake Duniani Mlimani City

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbord Slaa ambaye hivi karibuni alitamka kuwa atarejea katika chama chake cha zamani ameonekana leo katika siku ya wanawake duniani ambapo Baraza la Wanawake (BAWACHA) walimualika kushirikia maadhimisho hayo.

Wanawake waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wameshiriki na kuadhimisha siku hiyo katika mkoa Dar es salaam, katika ukumbi wa Mlimani City.