Dkt. Tulia: 2020 Nitagombea

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania,  Dkt. Tulia Ackson, amesema ana mpango wa kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2020, lakini hajabainisha atagombea jimbo gani, kwa kile alichodai chama chake cha CCM, kinamzuia kutaja jimbo atakalogombea.

 

“Mwenyezi Mungu akitupa uhai 2020 nitagombea, ila nitagombea wapi? Naomba watulie kwa sababu chama chetu kina utaratibu wake, ila nashukuru ninavyoonekana nina uwezo wa kugombea maeneo mengi,” amesema na kuongeza:

 

“Pale Mbeya mjini kuna ofisi ya Tulia Trust, kwa hiyo wananchi wakisikia umefanya maeneo mengine, pale Mbeya maombi yanakuwa ni mengi, lakini kuhusu watu kufikiri mimi nataka jimbo hilo, siwezi kusema chochote.”

 

CREDIT: EATV


Loading...

Toa comment