Dkt. Yahaya Nawanda Ashinda Kesi dhidi ya Mwanafunzi wa Chuo
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda ameachiwa huru baada ya kushinda kesi aliyokuwa akituhumiwa ya kumlawiti Mwanafunzi wa Chuo iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kesi ya Jinai Namba 18853 Jinai ya mwaka 2024 ambapo mashahidi 11 walitoa ushahdi wao.
Dkt. Nawanda alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.