The House of Favourite Newspapers

DNA kumaliza utata mtoto wa Diamond

Unakumbuka ule utata wa binti wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika; Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’, aliyemzaa mwaka 2015 na mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, kiasi cha kutakiwa kupima vinasaba (DNA)?

DNA (Deoxyribo Nucleic Acid) ni kipimo cha chembe hai za binadamu ambazo zinarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi ambazo hupatikana kwenye chembe hai nyeupe za damu. Kipimo hiki hufanyika katika maabara maalum na huchukua siku saba au zaidi kutoa majibu na moja ya sababu za kupima DNA ni kutambua matatizo ya kimaumbile (genetic disorder testing) au kutambua kama mwanafamilia amebeba virithishi kwenda kwa mtoto (carrier testing) na kujua mzazi halisi (paternity testing) wa mtoto.

Utata wa Tiffah sasa umejirudia kwa mtoto mwingine wa Diamond au Mondi aliyezaa na mtangazaji kutoka Kenya, Tanasha Donna hivi karibuni ambaye bado hawajamtangaza jina. Oktoba 2, mwaka huu, Mondi na Tanasha walijaaliwa mtoto wa kiume ambaye sasa anazua mjadala kila kona baada ya kuoneshwa sehemu ya kichwani na baadhi ya watu kudai kuwa ana nywele za Kiarabu.Image result for tanasha na diamond

Kama ilivyokuwa kwa Tiffah, baadhi ya wachangiaji wa mitandao wanadai kuwa jamaa huyo ‘amepigwa’ na Tanasha kwani mtoto hafanani naye, hivyo kitakachomaliza utata ni DNA tu. Habari kutoka kwa chanzo kilicho ndani ya familia ya Mondi zinadai kuwa, kutokana na madai hayo, wapo baadhi ya ndugu nao wanashinikiza kifanyike kipimo cha DNA ili kumaliza utata huo.

“Ni kweli hiyo ishu imeleta sintofahamu baada ya mama Mondi (Sanura Kassim ‘Mama Dangote’) kutupia vipande vya picha za mtoto huyo zinazoonesha sehemu ya kichwani. “Wapo wanaodai yule mtoto ana nywele za Kiarabu na wengine wanadai ni Singasinga hivyo kitakachong’amua kitendawili hicho ni vipimo vya DNA tu,” kilidai chanzo hicho.

Juma Lokole ni rafiki mkubwa wa familia ya Mondi ambaye yeye anasema ukweli kuwa mtoto ni wa Diamond. Gazeti la Amani lilizungumza na Mama Dangote na kumuuliza kuhusu madai hayo ya mtandaoni na kama ni kweli familia inashinikiza kupima DNA ambapo alikuwa na haya ya kusema kwa kifupi juu ya sakata hilo; “Na sisi tunaona tu kama ninyi mnavyoona mitandaoni. Kwa hiyo subirini mtaona.”

Amani: Tusubiri tutaona akibadilika na kufafa na Diamond au?

Mama Dangote: Mimi ninachowaambia subirini mtaona.

Hata hivyo, Gazeti la Amani linafahamu kuwa, Tanasha ni shombeshombe; yaani mchanganyiko wa mama Mjaluo wa Kenya na baba ambaye ni raia wa nchini Italia, hivyo kuna uwezekano mtoto huyo

Comments are closed.