Dogo Janja Alivyozua Taharuki Fiesta!

HATA ungekuwa wewe, ukimuona mtu unayemfahamu, mara paaap kazungukwa na polisi wenye silaha lazima taharuki ikushike; ndivyo ilivyokuwa kwa msanii Abdulraaziz Chende, a.k.a Dogo Janja au Janjaro.

 

Ijumaa iliyopita katika Tamasha la Fiesta lililofanyika Viwanja vya Posta jijini Dar, ishu ya Janjaro kuzungukwa na polisi ndiyo ilitokea ambapo baadhi ya watu waliohudhuria tamasha hilo walipoona hivyo wakajua kimemnukia.

 

“Kuna nini, kuna nini?” Zikawa kibao midomoni mwa watu kiasi cha kuzua taharuki kwa mashabiki wake ambao walionekana kutaka kujua msanii huyo amepatwa na janga gani hadi akazungukwa na polisi.

Awali lilioneka kuwa si tukio la kawaida kutokana na jinsi maafande hao waliokuwa na silaha walivyokuwa wamemuweka mtu kati, lakini baadaye ikaja kujulikana kuwa, hakukuwa na shida yoyote na kwamba kulikuwa na mazungumzo ya kawaida.

 

Janjaro ambaye wakati huo alikuwa kifua wazi alihitimisha kumtoa pepo wa hofu aliyekuwa amewaingia wafuasi wake kwa kuonekana akicheka sambamba na polisi wale.

 

Paparazi wetu ambaye alikuwepo eneo la tukio naye alipoona hakuna ishu kubwa hakuona sababu ya kumuuliza chochote msanii huyo ambaye baada ya kumalizana na polisi wale alionekana akiwa beneti na mdada mmoja ambaye hakufahamika mara moja.

Hivi karibuni Janjaro alidaiwa kumwagana na mke wake Irene Uwoya ambapo yeye hajajitokeza hadharani kuuwambia chochote mashabiki zake kuhusu masuala ya ndoa yake kuvunjika.

Loading...

Toa comment