Dogo Janja Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya

 

RAPA Dogo Janja amemtambulisha mchumba wake mpya kupitia akaunti yake ya instagram akimtakia heri ya sikuku ya kuzaliwa huku akimsindikiza na maneno matamu ya mahaba.

 

Katika akaundi hiyo ameweka picha ya pamoja na mpenzi wake huyo mpya akiwa sura haionekani vizuri na maelezo yanayosomeka ifuatavyo:  “Hakuna neno linaloweza kutosha katika kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu..mengine nitakuelezea chumbani.. Kula ushibe, Kisha kaza chaga… nakupenda sana❤️❤️❤️❤️ @quenlinnatotoo#BuddahBossPonDiLove”

 

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Dogo Janja na Irene Uwoya kuonekana hawana maelewano mazuri huku ikisemekana kwamba kidume huyo amepata mwanamke mwingine.

 

 

Ikumbukwe kwamba miezi kadhaa nyuma,  Dogo Janja alifunga ndoa na msanii wa Bongo Movie, mwanadada Irene Uwoya, ambapo ndoa hiyo ilidumu kwa kipindi kifupi sana. Kwa upande wao,  kila mmoja hajakiri kama wameachana au bado wapo kwenye mahusiano.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment