MAKALA: NYEMO CHILONGANI NA MTANDAO
MTU mwenye ndoto ya kuwa bilionea ni lazima awe na mawazo ya kibilionea. Huwezi kumuona mtu mwenye ndoto za kuwa mwalimu akiwa na mawazo mengi kuhusu utabibu. Huwezi kumuona injinia akiwa na mawazo mengi kuhusu sheria. Ni lazima uwe na mawazo mengi juu ya kile unachokitaka.
Mabilionea wengi huwa wanacheza na mawazo kwani kabla walikuwa na mawazo ya kuwa hivyo walivyo. Waliwaza
kama mabilionea, walifanya kazi kama watu ambao waliamini kuna siku wangekuwa mabilionea. Ili ufi ke pale unapotaka ni lazima uwe na mawazo ya kukufanya kufi kaunapopataka.
Mbali na mabilionea wengi nchini Nigeria, leo tunamwangalia bilionea mwenye umri wa miaka arobaini tu (dogo), Igho Sanomi.
Wakati wewe ukikaribia miaka hiyo, tena ukiwa umeajiriwa au kufi kiria zaidi kuwatajirisha wengine, mwenzako ameshatengeneza utajiri wa kutisha, anaogelea katika bwawa la utajiri, kama yeye ameweza, kwa nini wewe ushindwe? Au unafi kiri ana mioyo miwili na miguu minne?
Hapana! Yupo kama wewe, nguvu kama zako na ubongo kama wako. Huyu jamaa amezaliwa mwaka 1975 huko Agbor, Delta State nchini Nigeria. Ni mtoto wa tano katika familia ya aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Dickens Ogheneruemu ambaye pia alikuwa mcheza gofu mzuri miaka ya nyuma.
Kwa fedha alizopewa na baba yake, jamaa alianza kuutafuta utajiri katika umri mdogo wa miaka ya thelathini tu. Hakukuwa na urahisi kwenye kuupata utajiri huo kwani alitakiwa kuhangaika, kusafi ri huku na kule kuangalia
wenzake walikuwa wakifanya nini hadi akafanikiwa.
Sanomi ni kijana mchakarikaji, kila dili lililokuwa likija mbele yake alilifanyia kazi ilimradi apate fedha ya kuyaendesha maisha yake. Alijiingiza kwenye sekta mbalimbali kama mawasiliano, usafi rishaji kupitia meli, ujenzi na mambo mengine mengi ilimradi tu apate mafanikio na kuwa bilionea mkubwa.
Baada ya kuona kuna utajiri mkubwa kwenye mafuta, hakutaka kuchelewa, akajiingiza huko kwa kuamini kwamba naye angefanikiwa na kuwa bilionea.
Hakupata kazi sana kwa sababu tu alikuwa mzawa, akaanza kusafi risha mafuta kwa kutumia kampuni ya kusafi risha mafuta ya Cosmos Oil AG.
Biashara yake kubwa ilikuwa ni kusafi risha mafuta kwenda nje ya nchi kwa kutumia Bandari ya Harcourt Refi nery na mafuta yake mengi alikuwa akiyauza nje ya nchi kwa kushirikiana na Kampuni ya Uswisi ya Zug Switzerland.
Baadaye aliona kwamba alikuwa akiwapa dili kubwa Cosmos hivyo alichokifanya mwaka 2004 ni kuanzisha kampuni yake ya mafuta na gesi ya Taleveras ambayo ndiyo imempa utajiri mkubwa.
Kwa kuwa jamaa alijua utajiri wake umejifi cha katika uuzaji wa mafuta, akaamua kujitanua zaidi. Akatengeneza ofi si nyingi Uingereza, Uswis, Afrika Kusini, Dubai, Ivory Coast, Abuja na Lagos.
Baadaye, Forbes walimtangaza kuwa mfalme mkubwa wa mafuta kuliko wote nchini Nigeria kwani kwa mwaka alikuwa na uwezo wa kusafi risha mpaka tani milioni 100 za mafuta ya petroli, mafuta ya taa na mafuta ya ndege.
NI BILIONEA ANAYEJITOLEA
Baada ya kutajirika, Sanomi alianzisha mradi uitwao The Dickens Sanomi ambao lengo lake kubwa ni kuwanufaisha wanafunzi kwa kuandaa mashindano ya kuandika insha ambapo shule iliyokuwa ikishinda anaisaidia kwa kuipelekea kompyuta, vitabu na vitu vingine vingi vya kuwasaidia kielimu.
NI MTU MAKINI KUSAIDIA WATU WENGINE
Mwaka 2012, kwa kupitia mradi wake wa uokoaji, jamaa aliwasaidia waathirika wa mafuriko 10,000 kwa
kuwapa chakula, makazi na kuwahudumia kwa kila kitu nchini Nigeria.
NI MTU WA MICHEZO
Wakati Nigeria ikijiandaa kuandaa mashindano ya Africa Youth Athlets Championship mwaka 2010, Sanomi alijitolea
naira milioni 10 kupitia kampuni yake ya Taleveras.
TUNAJIFUNZA NINI KWAKE?
Hatujifunzi kuwa mabilionea tu bali kitu kingine ambacho ni cha msingi mbali na kujituma, kuwa mbunifu ni kurudisha kwa jamii sehemu ya kile tunachokipata.
Itakuwa haina maana kama utakuwa bilionea leo huku majirani zako wakilala njaa, itakuwa haina maana ukiwa bilionea huku majirani zako wakiwa na maisha mabovu.
Kama Sinomi aliona ana fedha na watu wanahitaji msaada na kuwasaidia, vipi kuhusu wewe? Unahisi ukiwa bilionea na ukawasaidia watu wengine utafi lisika? Hakuna kitu kama hicho.
UTAJIRI WAKE SASA
Jamaa ana fedha ndefu, anaingia kwenye orodha ya matajiri wakubwa nchini Nigeria kwa kushika namba kumi huku akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.3 (zaidi ya Sh.trilioni 2.6.)