The House of Favourite Newspapers

Dokii Wanaume wote ‘chenga’

0
Ummy Wencelaus ‘Dokii’

MUIGIZAJI kitambo kwenye tansia ya filamu Bongo, Ummy Wencelaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa anaona umri unazidi kusonga mbele siku hadi siku lakini wa kumuoa bado hajamuona na kwamba kila mwanaume
anayemuona hafai kuwa naye ‘cheng’a.

 

Akizungumza na Star Mix Dokii alisema kuwa, mambo yamebadilika sana kila mwanaume anayemtazama labda anafaa kuwa mume wake haingii akilini hivyo anajikuta miaka inasogea tu.

 

“Yaani nimejitathimini nimeona miaka inaenda sana na umri unazidi kuwa mkubwa mno, sasa nikiangalia mpaka sasa wa kunioa sijamuona kabisa maana wanaume wote nawaona chenga labda ningepata nafasi ya kuonana na Myweather (bondia) pengine angeweza kuwa mume wangu,” alisema Dokii

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply