The House of Favourite Newspapers

Domayo Amshusha Presha Pluijm

KIUNGO mkabaji wa Azam FC, Franky Domayo amemrejeshea matumaini kocha wake Mholanzi, Hans van Pluijm baada ya kupona na kuanza mazoezi mepesi ya binafsi. Domayo amerejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya miezi miwili akiuguza majeraha ya goti.

 

Kurejea kwa kiungo huo kutaimarisha kikosi hicho ambacho kitamkosa kiungo wake Mzibambwe, Tafadzwa Kutinyu aliyepata majeraha ya goti kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mpinduzi walipokutana na Simba huko Zanzibar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja Mkuu wa Azam FC, Philip Alando, alisema kiungo huyo ameanza mazoezi hayo mepesi wiki hii baada ya kupona majeraha hayo.

 

Alando alisema Domayo ameanza mazoezi baada ya daktari mkuu wa timu, Mwanandi Mwankemwa kumfanyia vipimo vya mwisho kabla ya kumruhusu yeye pamoja na mwenzake Joseph Kimwaga kupona majeraha ya goti. “Ni habari nzuri kwa mashabiki wa Azam kuwa wachezaji wao Domayo na Kimwaga wameanza mazoezi mepesi ya binafsi wiki hii kabla ya kuanza magumu ya pamoja na wenzao hivi karibuni.

 

“Tunafurahia kupona kwa wachezaji hao ambao wamepishana na Kutinyu ambaye yeye naye alipata majeraha ya goti mechi na Simba katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.

 

“Hivyo, Domayo na Kimwaga wataanza kuonekana uwanjani hivi karibuni katika michezo ya ligi baada ya daktari wetu kuwaruhusu kuanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzao,” alisema Alando.
Kotei

Comments are closed.