visa

Dora: Siwezi Kukurupukia Mtoto

MSANII kunako Tasnia ya uigizaji hapa nchini, Wansukule Zakaria ’Dora’ amefunguka Kuwa kwa sasa hana mpango wa kupata mtoto, bado anakula ujana.

 

Akizungumza na Gazeti la Amani, Dora amesema kuwa hataki kukurupukia kupata mtoto kwa sasa hivi eti kwa sababu ya mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa, kwa sasa hivi anatafuta maisha ili atakapojaaliwa mtoto, asiteseke.

“Siwezi kukurupukia mtoto kwa sababu ya mitandao, mimi nitapata mtoto pale ninapotaka mwenyewe na siyo watu wanavyotaka, hata muhusika mwenyewe (mchumba wangu) analitambua fika suala hili.

 

Kwa upande wangu naona wakati bado, siwezi kuja kuzaa mtoto wangu akaja kuteseka baadaye, kingine ujana bado sijaumaliza,” alisema Dora ambaye kwa sasa anatamba kwenye Filamu ya Kapuni.

STORI: KHADIJA BAKARI, AMANI
Toa comment