Audio: Ni Wewe na Namna Gani Kutoka Kwa Walid

Msanii Walid Ali mwenye umri wa miaka 25, amezaliwa June 13 mwaka 1992 nchini Somalia mji wa Chulah Cha Bai, mama yake akiwa ni raia wa Zimbabwe na baba yake akiwa ni raia wa Tanzania. Aliishi nchini Tanzania mpaka alipofika umri wa miaka saba (7) ndipo alipohamia nchini Holland (Amsterdam). Amekulia huko mpaka alipofikisha umri wa miaka 13, ndipo alipoanza kufanya shughuli zake za muziki.

 

Alianza Kwa kufanya muziki aina ya Rap na Hip Hop mpaka alipogundua uwezo wake mkubwa kwenye muziki wa Rn’B. Alifanya kazi kwa bidii akiwa kama msanii mchanga anaejitegemea, alipokosea hakuacha kujifunza na kujirekebisha mpaka alipoona yupo sawa kusimama mbele za watu na kuonesha kipaji chake.

Kwa uwezo wake mkubwa ameweza kufanya muziki aina ya Afro Pop akiimba kwa lugha ya kiingereza na kiswahili kitu ambacho kilimvutia msanii Patoranking na kuamua kumsajiri kwenye Record Label yake iitwayo Amari Music iliyopo nchini Nigeria na kuonesha matumaini ya kuja kuwa msanii mkubwa Africa.

 

Akiwa ameelekeza nguvu kubwa ya muziki wake nchini Tanzania, Walid yupo tayari kuonesha uwezo wake mkubwa na kuishangaza Africa na Dunia kwa ujumla kupitia kipaji chake.

Kwa sasa msanii yupo chini ya msanii wa Nigeria Patoranking kupitia lable yake ya


Loading...

Toa comment