The House of Favourite Newspapers

Drake Kugeuka MC Mwezi Ujao!

0

CALIFORNIA, MAREKANI | IJUMAA WIKIENDA

MARA baada ya kuzoa tuzo 13 za Billboard, mkali wa Hip Hop, Aubrey Graham ‘Drake’ amepata shavu la kuwa mshereheshaji ‘MC’ kwa mara ya kwanza katika tuzo za mpira wa kikapu (NBA) zitakazofanyika Jumatatu ya Juni 26 jijini New York, Marekani.

Juzikati staa huyo anayebamba na ngoma kibao ikiwemo One Dance alioshirikiana na Wizkid kutoka Nigeria, alikuwa katika Mgahawa wa Madeo pande za California na marafiki zake huku muda mwingi akiongelea atakavyopagawisha usiku huo wa tuzo.

Pia inaelezwa katika usiku huo wa tuzo, rafiki yake wa karibu kimuziki, Nicki Minaj anatarajiwa kupiga shoo ya nguvu.

Usiku wa kuamkia Mei 22, nchini Marekani zilifanyika sherehe za utoaji tuzo kubwa za muziki na filamu, Billboard Music 2017 ambapo rapa Drake aliibuka kuwa ‘The biggest winner’ kwa mwaka huu kwa kuweka rekodi ya kushinda tuzo 13, akimuondoa mwimbaji Adele aliyekuwa akishikilia rekodi ya kushinda tuzo 12.

Leave A Reply