Drake na Rihanna Kuachia Albamu zao Usiku wa Grammy
Drake na Rihanna
TUNAWEZA kusema ni swali kwamba, Je, Drake na Rihanna wataachia albamu zao mpya mwezi ujao?
Hii imekuja baada ya chanzo kimoja cha habari za burudani na mastaa cha HITS Daily Double, kuripoti kuwa masupastaa hao wanafikiria kuachia albamu zao mpya kwenye usiku wa historia wa tasnia muziki, ni usiku ambao Tuzo za 58 za Grammy zitafanyika, Februari 15 mwaka huu.
Kanye West yeye tayari amekwisha weka wazi kuwa ataachia rasmi albamu yake mpya ya Swish Februari 11 mwaka huu. Kama na hawa wawili nao wataachia basi kutakuwa na albamu tatu kali za masupastaa zikazoachiwa ndani ya mwezi mmoja zikiwemo Views From the 6 ya Drake iliyosubiuliwa kwa muda mrefu na ANTI ya Rihanna.