DRC Yataja Waliohusika Mauaji Balozi wa Italia

SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imewashutumu waasi wa FDLR wenye asili ya #Rwanda kwa shambulio lililosababisha mauaji ya Balozi wa #Italia nchini DRC, Luca Attanasio, aliyeuawa jana Februari 22, 2021.

 

Attanasio alikuwa katika msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na walishambuliwa karibu na Mji wa Goma, mashariki mwa Congo.

 

Hata hivyo, kundi la FDLR limekanusha kuhusika na shambulizi hilo kwa kile linachosema vikosi vyake viko mbali na eneo la shambulizi.

 

Maafisa katika Mbuga ya Wanyamapori ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara lililoshindikana.

 

Toa comment