The House of Favourite Newspapers

Droo Ndogo ya 4 ya Shinda Nyumba: Bila Mke Wangu Nisingepata Pikipiki

0
Mr. Shinda Nyumba (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi Shabani Ahmadi

 

WAKATI Bahati Nasi­bu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ikiende­lea katika hatua ya droo ndogo, ambapo wiki iliyopita ilichezeshwa ya nne, mshindi wa zawadi kubwa, Shabani Ahmadi Ngao ambaye ni mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, ametoa kauli ya kusisimua.

Ngao ambaye ni mso­maji wa muda mrefu wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa, Championi, Risasi, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda, siku zote hakuwahi kufikiri kama anaweza kupata ushindi kwa kujaza kuponi za bahati nasibu ya shinda nyumba, in­gawa tangu ianze ana­fahamu uwepo wake.

 

Mshindi, Shabani Ahmadi akimbeba mkewe kwenye pikipiki aliyoshinda

 

“Mimi nilikuwa niki­nunua gazeti nasoma vitu ninavyovihitaji ha­lafu naliacha naendelea na mambo yangu, sasa siku moja kumbe mke wangu naye alikuwa akiyasoma na akagundua kuwa nilikuwa sikati wala kujaza kuponi za shinda nyumba, akaniambia hata kama nadhani sitashinda lakini angalau nijaze tu kuliko kuziacha kuponi zipotee.

“Kwa kweli sikudhani kama naweza kushinda maana haya mambo bwana wakati mwingine mtu unashindwa kuamini, basi nikaan­za kujaza kuponi, sasa siku napigiwa simu kuwa nimeshinda, ikabidi nimtaarifu mke wangu ambaye alifurahi sana,” anasema Ngao.

 

Mr. Shinda Nyumba akiwakabidhi Shabani Ahmadi na mkewe ufunguo wa pikipiki

 

Kuonyesha kuwa mkewe alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa pikipiki aliyopewa kwa kuibuka mshindi wa zawadi kubwa katika droo ndogo ya nne, Ngao alifika katika hafla ya kukabidhiwa kifaa hicho cha moto akiwa ameon­gozana na mkewe, Leyla Alex.

“Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti ya Global kwa kipindi kirefu, lakini awali nilikuwa na­soma bila kujaza kuponi lakini huyu mke wangu ndiye aliyenihamasisha kukata kuponi na ku­shiriki mchezo huu.

 

“Ndiyo maana hata leo nikaona nisimuache nyumbani, bora nije naye ajionee mwenyewe jam­bo jema alilonishauri na kutimia, Mungu ambariki sana mke wangu Leyla,” al­isema Ngao ambaye baada ya kupewa zawadi yake, aliiwa­sha na kuondoka nayo akiwa amempakiza mkewe.

 

Washindi wote katika picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba

Licha ya Ngao, washindi wengine saba waliibuka na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na simu za kisasa aina ya Phantom 6, dinner set na watu wen­gine watano ambao walijishindia zawadi ya ving’amuzi kutoka Kampuni ya Ting.

Afisa Masoko wa Global Publishers Yohana Mkanda, aliyekuwepo katika ha­fla hiyo ya kuwakabidhi washindi zawadi aliendelea kusisitiza juu ya wasomaji kuendelea kukata kuponi kwenye magazeti hayo, wakati huu bahati nasibu hiyo ikielekea kunoga zaidi.

Mr. Shinda Nyumba akielezea furaha yake.

“Kwenye magazeti yetu yote, katika kurasa za pili zipo kuponi zenye maelek­ezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, unaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima au wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofisini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda.

Bahati Nasibu hii Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Tech­nology.

MAKALA: RICHARD BUKOS IJUMAA WIKIENDA

VIDEO: Washindi 8 wa Droo Ndogo Shinda Nyumba Wakabidhiwa Zawadi Zao

Leave A Reply