Droo Ndogo ya Nne Shinda Nyumba… Washindi Wapongeza Kukabidhiwa Ving’amuzi (Video)
DAR ES SALAAM: Baada ya washindi watatu wa droo ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili kupewa zawadi zao Jumanne, juzi walioshinda Ving’amuzi vya Ting, ambao ni watano, nao walikabidhiwa chao kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Global Publishers, Bamaga Mwenge jijini Dar.
Washindi hao walikabidhiwa zawadi hizo baada ya Peter Christopher Katua wa Ilala jijini Dar, kushinda seti ya vyombo (dinner set), Ally Halifa Kachenje wa Arusha (simu) na Shabani Ahmadi Ngao wa Tabata Dar aliyeibuka mshindi wa pikipiki kupewa chao.Mwakilishi wa TING, Caroline Collent (kushoto) akimkabidhi zawadi ya king’amuzi, Farida Mukhisin aliyekua kwa niaba ya Verus Kweyamba wa Moshi.
Washindi waliokabidhiwa zawadi zao ni Dokta Uhemba wa Dodoma, Verus Kweyamba wa Moshi, Ally Ramadhan wa Mburahati, Rhoda Kimenyi wa Morogoro na Ringo Mbuya mkazi wa Uyole mkoani Mbeya.
Hata hivyo, ni washindi watatu tu ndiyo waliojitokeza na kupewa zawadi zao, ambao ni Ally Ramadhan Kazi, Verus Kweyamba na Rhoda Kimenyi. Ambao hawakutokea ni Dokta Uhemba na Ringo Mbuya ambao utaratibu mwingine utafanyika juu ya kupewa zawadi zao.Mkuu wa Idara ya Usambazaji ya Global Publishers, LawranceKabende akimkabidhi zawa ya King’amuzi cha TING, Mary Mboya aliyechukua kwa niaba ya RhodaKimenyiwa Mrogoro.
Afisa Masoko wa Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda, Yohana Mkanda, alisema zoezi hilo limehitimisha shughuli za droo ndogo ya nne, i l i yofany i k a wiki mbili zilizopita katika Viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar.
“Hapa sasa tumekamilisha zoezi letu kuhusu droo ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, niwaombe wasomaji wa magazeti yetu kuendelea kutuunga mkono kwa kununua na kujaza kuponi na kuzituma kwetu kupitia mawakala wetu walio nchi nzima, kama kuna tatizo la namna ya kuwapata, tafadhali wawasiliane nasi kupitia namba zinazopatikana kwenye magazeti yetu yote kwa maelekezo zaidi,” alisema Mkanda.
Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.