PIKIPIKI ya tatu kutolewa tangu kuanza kwa droo ndogo za Shinda Nyumba awamu ya pili itatolewa leo katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam.
Sambamba na pikipiki hiyo mpya kabisa, zawadi zingine zitakazotolewa ni pamoja na simu za kisasa kabisa smartphone, seti ya televisheni na dinner set.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema kuwa droo hiyo itachezeshwa katika viwanja hivyo kuanzia saa nane mchana hadi 12 jioni.
“Mipango yote kwa ajili ya shughuli hiyo imekamilika, tunawaomba wasomaji wetu kuendelea kuhifadhi kuponi zao na kujitokeza kwa wingi siku ya droo, kwani kama tulivyoahidi, zawadi kemkem zitatolewa na washindi watatangazwa mubashara,” alisema Mkanda.
Droo hiyo ndogo ya tatu itafanyika baada ya mbili za awali, ambazo washindi walipata zawadi kama hizo. Droo ya kwanza ilifanyika ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na ya pili ilifanyika katika Viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwanayamala.
Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda, ni kampuni pekee ya uchapaji magazeti kuwahi kutoa zawadi kubwa ya nyumba katika bahati nasibu.
Ili kupata kuponi hizo, msomaji anatakiwa kununua mojawapo ya magazeti ya kampuni hiyo na kujaza kuponi zilizopo katika ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzipeleka kwa mawakala waliopo nchi nzima na kwa wale wa Dar, wanaweza kupeleka ofisi za Global Publishers, zilizopo Bamaga, Mwenge.
Bahati Nasibu hiyo ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, imedhaminiwa na British School waliopo karibu na kituo cha daladala cha ITV na Kanisa la Lutheran Mwenge na Kilimanjaro Institute of Technology waliopo Mwenge kwa Mama Ngoma na Sinza Mori.