The House of Favourite Newspapers

Droo ya CAF Yatoka Rasmi, Yanga na Simba Zatambua Wapinzani Wao

0

 

Yanga SC

KLABU ya Yanga imepangwa kucheza dhidi ya Klabu ya Zalan FC ya nchini Sudan Kusini katika hatua ya raundi ya awali ya mashindano ya klabu bingwa Barani Afrika.

Zalan FC

Mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kukutana na mshindi kati ya mchezo wa St George ya nchini Ethiopia dhidi ya klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan.

Simba SC

Michezo yote ya hatua ya awali ya mtoano ya kufuzu kushiriki raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika itaanza kuchezwa Septemba 9-11 na marudiano Septemba 16-18 huku michezo ya raundi ya kwanza ikichezwa kati ya Okoba 7-9 na marudiano ni Oktoba 15-16.

Nyasa Big Bullets

Aidha Klabu ya Simba imepangwa dhidi ya klabu ya Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi ambapo mshindi baina wa mchezo huo atavaana na mshindi wa mchezo kati ya Red Arrows ya nchini Zambia dhidi ya Primeirode Agosto ya nchini Angola.

Leave A Reply