The House of Favourite Newspapers

Droo ya Kwanza ya Shinda Nyumba Yaunguruma – Dar

0

Nyumba (1)MC  Chaku (kushoto ) akiandaa kofia kwa mshindi wa droo ndogondogo za awali kabla ya droo ya kwanza ya shindano la bahati nasibu la Shinda Nyumba itakayochezeshwa leo jioni kwenye Viwanja vya Mbagala Zakhem – Dar.Nyumba (2)Mshindi akipokea zawadi ya kofia na kupongezwa na Afisa Usambazaji wa Global Publishers,  Jordan Ngowi (kulia), Temeke Mwembe Yanga ambapo jioni ya leo droo ya kwanza itachezeshwa Viwanja vya Mbagala Zakhem.NYUMBA (1)Mmoja wa wananchi aliyefika kwenye gari la kuchezesha droo ya awali mapema leo akichukua kuponi ndani ya ndoo ili kumpata mshindi wa zawadi za awali.NYUMBA (2)Wasomaji wakichangamkia magazeti ya Global kushiriki ‘Shinda Nyumba’.
Nyumba (3)Gari la matangazo likiwa eneo la Temeke Mwembe Yanga tayari kwa kuelekea viwanja vya Mbagala Zakhem ambapo droo ya kwanza ya Shinda Nyumba itachezeshwa jioni ya leo.

Mapema leo asubuhi, wakazi wa maeneo ya Temeke Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam wameonekana kuchangamkia kununua gazeti la Amani linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers ili kushiriki droo ya kwanza ya Shinda Nyumba.

Mbali na kuchangamkia gazeti hilo pia MC  Chaku, wa bahati nasibu hiyo amechezesha droo za awali na baadhi ya wasomaji kujipatia zawadi kama kofia na fulana.

Droo ya kwanza ya shindano la bahati nasibu la Shinda Nyumba itachezeshwa leo jioni kwenye Viwanja vya Mbagala Zakhem – Dar.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply