The House of Favourite Newspapers

Droo ya Nne ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Huu

0
Edna (kushoto) na Rukia wakiuza magazeti ya Global eneo la Ubungo mataa.  

DROO ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imewadia na sasa itafanyika mwezi huu kwa washindi kupata zawadi mbalimbali ikiwemo kubwa ya pikipiki.

Mr Shnda Nyumba (katikati) akiwa na waendesha bodaboda wa Kibamba shule.

Afisa Masoko wa Global Publishers, inayoendesha bahati nasibu hiyo, Yohana Mkanda alisema kuwa baada ya kufanya droo ndogo tatu kwa mafanikio HIYOOO Droo ya Nne Shinda Nyumba makubwa, sasa inakuja ya nne ambayo itafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika eneo ambalo bado linafanyiwa kazi.

“Tuna uhakika wa kufanya droo hiyo mwisho wa mwezi huu, lakini kuhusu wapi tutalifanyia zoezi hilo, bado tunaendelea na mazungumzo na mara tu itakapokamilika, tutawafahamisha wasomaji wetu ili wakae mkao wa kula tayari kwa shughuli hiyo.

Madereva bodaboda wakiendelea kujaza kuponi.

“Kama wanavyojua tumeanza kuboresha zawadi zetu kwa kadiri tunavyokwenda, katika droo zetu tatu ndogo ambazo tumeshazifanya, jumla ya pikipiki tatu zimeshatolewa, televisheni kubwa flat screen tatu pia, dinner set tatu na simu za kisasa nyingi tu.

“Tunawasihi waendelee kusoma magazeti yetu ambayo licha ya bahati nasibu hiyo, pia yanawaletea habari motomoto za kijamii, michezo, burudani na mastaa mbalimbali.

“Kwenye magazeti yetu yote, katika kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, unaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima na wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofisini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda. Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Mr Shinda Nyumba akiendelea kuongea na wasomaji wetu.

Leave A Reply