The House of Favourite Newspapers

Droo ya pili ya Shinda Nyumba kufanyika leo Dar

0

21.Mmoja-wa-abiria-aliyekuwa-akisafiri-eneo-la-Ubungo-stendi-ya-mabasi-akiweka-kuponi-yake-kwa-ajili-ya-kushiriki-bahati-nasibu-ya-shinda-nyumba-na-Global-Publishers.BAADA ya kufanyika kwa droo ya kwanza iliyowanufaisha wasomaji wa Magazeti ya Uwazi,Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, leo (Februari 18) kutachezeshwa droo nyingine ya pili ya Shinda Nyumba maeneo ya Mchikichini-Karume jijini Dar.

Akizungumza na Amani, Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema ili kuweza kushiriki katika droo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ni kununua gazeti lolote linalochapwa na Global Publishers na kujaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili itakayokuwezesha kushiriki.

“Tunatarajia kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo televisheni ‘flat screen’ na ving’amuzi vya TING, vyombo vya jikoni, mashuka na zawadi zingine kibao, aidha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki,” alisema Mkanda.

Leave A Reply