The House of Favourite Newspapers

Droo ya Robo Fainali UEFA na EUROPA Kupangwa Leo

0

DROO ya kupanga klabu ipi kukutana na ipi kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ‘Uefa Champions League” na michuano ya Europa inataraji kupangwa saa 8:00 mchana wa leo tarehe 19 Machi 2021 kwenye mji wa Nyon nchini Uswizi.

 

 

Droo hiyo inatakayochezeshwa kwenye ofisi za makao makuu ya shirikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’, itaanza kwa kupanga michezo ya robo fainali ya michuano hiyo na lisaa moja baadae droo ya michuano ya Europa itafuatia.

 

 

Timu nane zilizofuzu hatua ya rbo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya zinazosubiri kuchezeshwa kwenye droo hiyo ni vilabu vya, bingwa mtetezi, Bayern Munich, Borussia Dortmund zote za Ujerumani, makamu bingwa PSG ya Ufaransa, FC Porto ya Ureno na Real Madrid ya Hispania.

 

 

Vilabu vingine ni Chelsea, Manchester City na Liverpool kutoka nchini England, na kuifanya ligi hiyo kuwa ligi pekee iliyotoa vilabu vitatu vilivyotinga hatua hiyo kwa msimu huu.

 

 

Kwa upande wa michuano ya Europa ambayo michezo yake ya hatua ya 16 bora imetamatika usiku wa kuamkia leo kwa Manchester United kufuzu kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AC Milan na kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.

 

 

Arsenal ilipoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki, lakini Gunners walifuzu baada ya kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mchezo wa kwana kupata ushindi wa mabao 3-1 ugenini.

 

 

Mchezo uliokuwa na matokeo ya kushangaza ni ule ulioshuhudiwa Dynamo Zagreb ya nchini Croatia ikipindua matokeo ya kufungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza na Tottenham Hotspurs ya England na usiku wa jana kupata ushindi wa mabao 3-0 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare 2-2.

 

 

Shujaa wa mchezo huo ni Mislav Orsic aliyefunga mabao yote matatu ‘Hat trik’ na kumuacha kocha wa Spurs, Jose Mourinho kubaki akiwatupia lawama wachezaji wake kwa kukosa umakini.

 

 

Vilabu vingine vilivyotinga robo fainali ya michuano ya Europa ni AS Roma ya Italia, Ajax ya nchini Uholanzi, Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech, Granada na Villarreal zote za kutoka nchini Hispania.

 

 

Baada ya droo hiyo kupangwa mchana wa leo, michezo ya mkondo wa kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itataraji kuchezwa tarehe 6 na 7 mwezi Aprili mwaka huu na ile ya mkondo wa pili kupigwa tarehe 13 na 14 mwezi Aprili 2021 huku nusu fainali ikiwa 27 na 28 Aprili 2021.

 

 

Michezo yote nane ya robo fainali ya Europa inatazamiwa kuchezwa tarehe 8 kwa ile ya mkondo wa kwanza na mkondo wa pili kuchezwa tarehe 15 Aprili mwaka huu huku nusu fainali ikitazamiwa kuchezwa tarehe 29 April 2021.

 

 

Fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepangwa kuchezwa tarehe 29 Mei 2021 kwenye dimba la Ataturk Olympic nchini Uturuki ilhali ile ya Europa kuchezwa tarehe 26 Mei 2021 kwenye dimba la Gdansk Arena nchini Poland.

Leave A Reply