The House of Favourite Newspapers
gunners X

Droo ya 6 ‘Tusua Maisha na Global’, Erasto Ajishindia Pikipiki – Video

MAMBO yanazidi kunoga katika Shindano la’ Tusua Maisha na Global’ ambapo droo ya sita  imefanyika jana kupitia Global TV Online ambayo ni runinga ya mtandaoni inayopatikana Youtube ambapo Erasto Luponelo wa Makambako, Njombe,  aliibuka  mshindi wa sita wa pikipiki.   Victor Lucas kutoka Tanga alijishindia jezi orijino ya timu mojawapo ya Uingereza.

 

Wengine ni Erasto Omary wa Boko jijini Dar aliyejishindia Headphone za kisasa za Beats by Dre na Augustine Haule wa Kinyerezi jijini Dar aliyejishindia vyombo vya maakuli (dinner set).

Droo nyingine  ya saba inatarajiwa kuchezeshwa wiki ijayo Jumanne.  Ili kushiriki shindano hili,  unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti yanayotoka katika kampuni ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Mchanganyiko, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Spoti Xtra na Champion.  Baada ya kununua moja kati ya magazeti hayo,  ndani yake utakuta kuponi;  ijaze na kisha ufuate maelekezo ili uweze Kutusua Maisha na Global.

Comments are closed.