The House of Favourite Newspapers

Droo ya tatu ya ‘Shinda Nyumba’ yachangamkiwa Tabata

1

1Adamu Hassan (katikati) akijaza kuponi yake baada ya kununua gazeti la Amani kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Global,Theresia Julian (kulia).

2 Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda (wa tatu kulia) akiwaelekeza wasomaji wa Gazeti la Amani namna ya kujaza kuponi zao.

3 Msomaji wa Amani aliyejitambulisha kwa jina la Daudi Ndangoba (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa ofisa masoko wa Global kabla ya kujaza kuponi yake.

4Ndamgoba akiweka kuponi yake kwenye ndoo maalum ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

5Harakati za kujaza kuponi zikipamba moto kushiriki droo ya tatu ya Shinda Nyumba.

6Kuponi zikiendelea kuwekwa kwenye ndoo maalum ya bahati nasibu.

7Juma Hamis (kushoto) akijaza kuponi yake huku ofisa wa Global, Yohana Mkanda akifuatilia zoezi hilo.

8 Msomaji wa Amani mkazi wa maeneo ya Tabata Migombani, Denis Mtajuka (kulia) akijaza kuponi yake.

9Wasomaji wakiendelea kujaza kuponi za kushiriki droo hiyo.

10 Mdau wa magazeti ya Global Publishers Ltd, Salome Lema (kushoto) akijaza kuponi yake kushiriki droo ya tatu ya Shinda Nyumba.

11 Msomaji wa Amani, Marystella Munishi (kushoto) akimpatia kalamu ofisa masoko wa Global ili aweza kumsaidia kujaza kuponi yake.

12..Akiweka kuponi yake kwenye ndoo.

13Wasomaji wa magazeti ya Global wa eneo la Tabata Kinyerezi wakipata maelekezo kutoka kwa ofisa masoko wa Global kabla ya kujaza kuponi zao.

14Wasomaji wa Gazeti la Amani wa eneo la stendi ya daladala ya Kinyerezi wakishiriki zoezi la kujaza kuponi.

15

Juma Abdalla (katikati) akijaza kuponi yake.
16

Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kushoto) akiikagua kuponi ya msomaji, Ummy Shaban (kulia) .

17Msomaji wa Magazeti ya Global, Sprian Agustino (kulia) akinunua gazeti kwa muuzaji ili kushiriki droo ya tatu ya Shinda Nyumba.

WASOMAJI wa magazeti ya Global Publishers Ltd wa maeneo ya Tabata-Migombani jijini Dar es Salaam na maeneo mengine, leo wameonekana kuichangamkia Bahati Nasibu hiyo inayoendelea hapa nchini kwa kununua gazeti la Amani na kujaza kuponi ya kushiriki droo ya tatu ya ‘Shinda Nyumba’.

Mara baada ya timu nzima inayozunguka maeneo mbalimbali hapa nchini kuhamasisha bahati nasibu hiyo kutua maeneo ya Tabata-Migombani na maeneo mengine, wasomaji wa Amani walijitokeza kwa wingi na kununua gazeti hilo kisha kujaza kuponi zinazopatikana kwenye ukurasa wa pili katika gazeti hilo huku pia wakijipatia zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema:  “Wanachotakiwa kufanya wakazi wa Tabata na maeneo mengine ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti  ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa 500/= na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa, kila anayejaza kuponi nyingi anajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba na zawadi nyingine,” alisema.

(Na Denis Mtima/Gpl)

1 Comment
  1. edwin fweni says

    droo ya tatu ndo final or kunanyingine?

Leave A Reply