The House of Favourite Newspapers

DSTV Yazindua Punguzo Kubwa Bei ya Vifurushi Dar -Video

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice, Tanzania, Jacqueline Woiso (kulia) akiongea jambo na msanii wa Bongo Fleva mwanadada Lulu Diva usiku wa jana Septemba 3, 2019, katika uzinduzi wa punguzo la bei kwa vifurushi vya DStv katika hoteli ya The Terrence Slipway jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma zake za DStv usiku wa Septemba 3,  2019, imezindua punguzo la bei kwa vifurushi vyake katika hoteli ya The Terrence Slipway jijini Dar es Salaam.

Wateja wamepokea kwa furaha hatua hiyo hasa ikizingatiwa kuwa punguzo hilo kubwa la bei haliathiri maudhui katika vifurushi vya DStv.

Bei hizo mpya zilizoanza kutumika tarehe 1, Septemba, mwaka huu,  zimepungua kwa kiasi kikubwa huku baadhi ya vifurushi ikiwa ni punguzo la zaidi ya 30% ikilinganishwa na bei ya awali.

Meneja wa Masoko wa MultiChoice Tanzania,  Ronald Baraka Shelukindo,  akiongea jambo katika uzinduzi huo.

Bei hizo mpya zinaonyesha kuwa kifurushi cha DStv Premium kitakuwa na punguzo la Sh 40,000 kutoka bei ya sasa ya Sh 169,000 hadi 129,000; Kifurushi cha DStv Compact+ punguzo la Sh 25,000 kutoka 109,000 hadi 84,000;  Kifurushi cha DStv Compact punguzo la Sh 25,000 kutoka 69,000 hadi  44,000; na kifurushi cha DStv Family punguzo la Sh 10,000 kutoka 39,000 hadi 29,000.

Mabadiliko hayo yanakuja muda mfupi tu baada ya kuanza kwa msimu wa soka ambapo ligi kubwa maarufu duniani zimeanza hivyo kuwawezesha wateja wa DStv kushuhudia ligi hizo kwa bei nafuu.

Akizungumza katika hafla maalum ya kutangaza bei hizo mpya kwa wadau na wateja wa DStv iliyofanyika Slip way jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso, amewahakikishia wateja wa DStv kuwa kushuka huko kwa bei hakutasababisha mabadiliko ya chaneli katika vifurushi hivyo mteja ataendelea kupata chaneli zilezile alizokuwa akipata awali ila sasa atakuwa analipa bei ndogo zaidi.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kushoto) akisalimiana na William Malecela ‘Le Mutuz Super Brand’.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo, baadhi ya wasanii ambao walishiriki katika hafla hiyo wamepongeza uamuzi huo ambao wamesema ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na wateja wa DStv.

 

Mwanamuziki maarufu Jo Makini amesema kitendo cha DStv kupunguza bei hususan ya kifurushi cha Compact ambacho huonyesha mechi zote za baadhi ya ligi kubwa duniani ikiwemo ile ya Uingereza EPL kutoka Sh 69,000 hadi Sh 44 ni habari njema sana kwa wapenda soka hapa nchini

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Joh Makini (kushoto) akisalimiana na Saleh Ally.

Naye Lulu Diva, mwanamuziki na muigizaji maarufu wa tamthilia ya Rebeka, amesema kuwa kwa bei hizo mpya wapenzi wa sinema na tamthilia mbalimbali sasa hawana sababu ya kukosa uhundo huo kupitia DStv kwani bei zimekuwa rafiki zaidi.

Mchekeshaji Pierre Konki Liquid (aliyenyoosha mkono) akiongea neni katika uzinduzi huo

Mwanamuziki maarufu nchini Mwana FA naye aliungana na wenzake kuelezea furaha yake kwa kupungua huko kwa bei za vifurushi vya DStv.

“Kwa kweli sasa DStv imekuwa nafuu sana na hii ina maana Watanzania wengi zaidi wataweza kupata habari na burudani kabambe kutoka DStv kwa gharama nafuu kabisa,” alisema.

Msanii wa muziki Bongo, Quick Rocka (kulia) akipiga ‘selfie’. Katikati ni Lulu Diva na Joh Makini.

Comments are closed.