Kartra

DStv Yaja na Zigo Kama Lote

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania (DStv) imetangaza kuzindua rasmi kifurushi kipya cha bei nafuu kijulikanacho kama DStv Poa na kinapatikana kwa gharama ya shilingi 9,900 tu kwa mwezi ambapo kimeanza kutumika kuanzia Septemba 1, 2021.


Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema kuanzishwa kwa kifurushi hicho kutawafanya wateja Watanzania kuwa na wigo mpana wa kuchagua kifurushi wanachokitaka kulingana na uwezo wao.

 

“Kuanzishwa kwa kifurushi hiki kunaendana na kipaumbele chetu cha kuwajali wateja na kuwapatia huduma bora kwa gharama nafuu kadiri iwezekanavyo.

Tunatambua kuwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla wanapitia wakati mgumu kiuchumi, hivyo tumetathmini njia bora za kuhakikisha kuwa Watanzania wanaendelea kupata burudani, habari na elimu kwa gharama nafuu zaidi,” amebainisha Jacqueline.

 

Amesema kuwa, mbali na kifurushi cha DStv Poa kuwa cha gharama nafuu sana, kifurushi hicho pia kimesheheni chaneli motomoto zaidi ya 40 za habari, filamu, michezo na burudani kedekede kuendana na matakwa ya wateja wetu.

Sambamba na kifurushi hicho, pia DStv imeanzisha chaneli mpya ya Maisha Magic Poa itakayokuwa na vipindi kabambe kama vile ‘Ni Yeye’ kinachoongozwa na wasanii maarufu TID na Chid Benz, Vichekesho vya Watu Baki, Kipindi maarufu cha vichekesho cha Origino Comedy bila kushahau tamthilia za Kapuni, Sarafu, Mwantumu na Sinema bora za Mambo Moto.

 

Akitoa maelezo kuhusu kifurushi hicho kipya, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo alisema kuwa kutokana na wingi wa chaneli zilizopo kwenye kifurushi hicho na maudhui yake, wateja wa DStv watarajie ‘zigo’ la burudani.

 

“Hili ni zigo kwelikweli kwani kuna chaneli zaidi ya 40, na zote hizi kwa bei ya Shilingi 9,900 tu kwa mwezi,” alisema.

Amesema habari njema zaidi ni kwa wateja wa DStv ambao akaunti zao zina salio linalotosha kuwashiwa kifurushi hicho, kwani ikiwa wataridhia, wataunganishwa na kifurushi hicho cha DStv Poa kwa shilingi 9,900 tu na kuendelea kufurahia burudani kutoka DStv na kwa mteja mpya ataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 59,000 tu


Toa comment