The House of Favourite Newspapers

DStv Yazindua Msimu Mpya wa ‘Soka Mwanzo Mwisho’!

VUGUVUGU la msimu mpya wa soka linazidi kupamba moto huku maelfu ya mashabiki wa soka kote nchini wakisubiri kwa hamu tangazo kutoka DStv ili kujua kuwa je, bado wataendelea kupata uhundo wa ligi maarufu duniani kupitia DStv?

 

Swali hilo limepata jibu baada ya MultiChoice kutangaza rasmi kuwa king’amuzi cha DStv kitarusha mubashara mitanange ya ligi maarufu ulimwenguni ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Ligi ya Italia (Serie A ), Ligi ya Hispania (La Liga), Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) pamoja na makombe mengine maarufu duniani.

 

Pazia la msimu huu mpya wa soka litafunguliwa Agosti 4, mwaka huu kwa mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Liverpool na kigogo wa ligi ya Uingereza, Manchester City mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia DStv.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar, Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, alisema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuendelea kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia ligi ya Uingereza itakayorushwa kwa Lugha ya Kiswahili.

 

“Kampeni yetu ya sasa tunasema ni ‘Soka Mwanzo Mwisho’ na tunamaanisha kwani kwa wateja wetu wa DStv. Ni wapi unaweza kuona mechi zote 380 za Ligi ya Uingereza, mechi 380, za Ligi Kuu ya Hispania, mechi 380 za Ligi Kuu ya Italia bila kusahau mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na nyingine nyingi?

 

“Katika kuhakikisha kuwa burudani hiyo haimpiti mteja wa DStv, kwa kupitia App ya DStv Now wateja wataweza pia kuangalia popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, tablet na laptop.

 

“Mteja anayetumia DStv Now anaweza kuunganisha vifaa vinne tofauti kwa kutumia akaunti moja bila malipo ya ziada.” Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wadau wa soka nchini wakiwemo wasanii mbalimbali, wachezaji wastaafu na watangazaji wanaotangaza Ligi Kuu ya Uingereza kwa Kiswahili ambao ni Salama Jabir, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Abuubakar Lyongo na Oscar Oscar.

 

Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo, DStv pia imetangaza ofa maalum kwa wateja wapya wanaojiunga kuanzia Agosti Mosi, 2019 hadi Septemba 30, 2019 watajiunga na DStv kwa Sh 99,000/ na kupata kifurushi cha Family kwa miezi miwili.

Comments are closed.