The House of Favourite Newspapers

DSTV yazindua msimu mpya wa soka, Premier kutangazwa kwa Kiswahili

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Mria, akizungumza jambo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania.
Ephraim Kibonde (kushoto) na Aboubakar Liongo ni miongoni mwa watangazaji watakaotangaza Ligi ya England kwa Kiswahili.
Abdallah Kanini ambaye ni moja wa washindi waliojishindia King’amuzi (kulia) akipewa zawadi yake.
Denis Mtima (kulia) ambaye ni mwandishi wa Global Publishers akipewa zawadi yake baada ya kuibuka mshindi kwenye droo iliyochezeshwa maalum kwa ajili ya waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo.

 

 

WAKATI vuguvugu la soka ulimwenguni likizidi kupanda, Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia King’amuzi cha DSTV, imezindua kampeni maalum ya msimu mpya wa soka ijulikanayo kama ‘Full Vyenga Bila Chenga’ ambapo Watanzania kupitia DSTV wataweza kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguni inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi Kuu ya England (Premier), Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu duniani.

Pazia la Premier litafunguliwa Jumapili ya Agosti 6 kwa mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia DSTV.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika Ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Maharage Chande, amesema kuwa msimu huu wa soka, DSTV inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika mwonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa Lugha ya Kiswahili.

 

Msimu huu Watanzania kupitia DSTV, siyo tu kwamba wataona mubashara michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa Watanzania kufuatilia Ligi Kuu ya England kwa Lugha ya Kiswahili,” alisema Chande.

 

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga Bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DSTV, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka kwa mwonekano bora zaidi, yaani bila chenga.

 

“Tunatambua kuwa washabiki wa soka sasa wanataka walione soka vyema kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DSTV, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘Full Vyenga Bila Chenga’ kwenda mbele,” alisema Alpha.
 
NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave A Reply