The House of Favourite Newspapers

DStv yazindua msimu mpya wa soka

0

Wakongwe wa soka nchini watoa rai

Dar es Salaam, 26 August 2020, – SuperSport ambayo ni maarufu kwa kurusha mubashara michezo mbalimbali duniani imetangaza kuzinduliwa rasmi kwa Msimu wa Soka ambapo sasa maandalizi ya ligi kubwa na maarufu duniani yamekamilika na ligi hizo zitaanza siku chache zijaro.

Kwa upande wa Tanzania uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam na kuhuduriwa na wadau mbali mbali wa soka wakiwemo wachezaji wakongwe waliocheza katika ligi kuu ya Tanzania pamoja na timu ya taifa – Taifa Stars kwa miaka mingi.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema DStv kwa kupitia chaneli za SuperSport kama kawaidia yake msimu huu watawaletea watanzania burudani hiyo mubashara na kwamba tofauti na miaka iliyopita, hivi sasa chaneli za SuperSport zimepangwa upya kulingana na aina ya mchezo unaoonyeshwa.

“Safari hii DStv na SuerSport tunakuletea Soka Lisilopimika! Tumejipanga vizuri zaidi na mbali ya kukuletea michuano mikubwa ulimwenguni kama ligi kuu ya Uingereza – EPL, Ligi kuu ya Hispania – La Liga ana nyinginezo, sasa chaneli za SuperSport zimepangwa mahususi kulingana na aina ya mchezo unaoonyeshwa. Kwa msingi huo sasa kutakuwa na chaneli mahususi kwa ajili ya ligi kuu ya Uingereza, chaneli mahususi kwa ligi ya Hispania, chaneli mahususi kwa Ligi ya Italia na kadhalika” alisema Shelukindo.

Shelukindo amesema kuwa mbali na ligi hizo tatu kubwa ulimwenguni, SuperSport itaendelea kuonyesha mashindano mengine makubwa duniani kama Euro 2020 Championship, UEFA Euro 2020 Qualifiers, European qualifiers kwa ajili ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, UEFA Champions League na UEFA Nations League.

“Mwaka huu kwa kweli kutakuwa na burudani ya aina yake ndani ya DStv na mipango tayari imeshakamilika na punde tu hali itakaporuhusu tutaanza kurusha ligi hizo kubwa kwa lugha ya Kiswahili kupitia SuperSport” alisisitiza Shelukindo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo wachezaji wakongwe hapa nchini akiwemo Edibily Lunyamila, Fikiri Magoso, Dua Said, Iddi Moshi, Sekilojo Chambua, Bakari Malima, Jumanne Njovu, Salvatory Edward, Mohamed Hussein Mwanamtwa Kihwelu na Ivo Mapunda wamesema wakati umefika kwa watanzania kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao wako juu ki soka ili na sisi tuweze kufikia viwango hivyo. Wamesema kuonekana kwa ligi kubwa duniani mubashara hapa Tanzania kuwe ni chachu ya kujifunza kutoka kwa wenzetu ili tuimarishe soka letu na hatimaye na sisi tuwe katika viwango kama walivyofikia wao.

Kutokana na kuchelewa kukamilika kwa msimu uliopita, ligi hizo maarufu duniani – Premier League, La Liga na Serie A  zitaanza mwezi Septemba ambapo Ligi kuu ya Uingereza na ile ya Hispania zitaanza Septemba 12 wakati ile ya Italia itaanza Septemba 19.

Ligi ya Uingereza inashuhudia ujio wa timu kama Leeds United, West Bromwich Albion na Fulham wakati kule Italy, Benevento na Crotone nazo zimepanda daraja ni hivyo kuingia Serie A. Kwa upande wa La Liga, Cadiz na Huesca ndiyo ingizo jipya kwenye ligi hiyo msimu huu.

Leave A Reply