The House of Favourite Newspapers

DTB-TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA.

Mkurugenzi wa fedha DTB Tanzania, Joseph Mabusi akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka DTB-Tanzania

Diamond Trust Bank (T) Ltd, (DTB-Tanzania) leo hii, imekabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Amana, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za kijamii. DTB-Tanzania kila mwaka hutenga asilimia 2% ya faida yake kwa ajili ya utekezaji wa shughuli za kijamii. Fedha hizi huelekezwa katika kuboresha huduma katika sekta za Afya, Elimu na Mazingira. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji.

Vyote hivi vikiwa na thamani ya Tshs 10,000,000.00. Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Dk.Kilomoni  alishukuru uongozi wa DTB-Tanzania kwa urafiki uliopo kati ya taasisi hizi mbili ambapo kila mwaka, DTB-Tanzania hutoa msaaada kama huo kwenyeb Hospitali hiyo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dk. Amim Kilomoni (wa pili kushoto) na Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Anna Musa (kushoto) wakisalimiana na wafanyakazi wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa pili kulia) na Sylvester Bahati (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka Benki hiyo

Naye Mkurugenzi wa fedha wa DTB-Tanzania, Ndg. Joseph Mabusi, akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano alisema, “kama taasisi ya kifedha kamwe hatuwezi kusahau jamii. Ni Dhahiri kwamba faida yetu hupatikana katika kufanya biashara na jamii inayotuzunguka. Kwa mtizamo huo, kila mwaka DTB-Tanzania hutenga fedha ambazo hutumika kwenye shughuli kama hii ya leo”.

Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa, akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa DTB Tanzania

Ngd, Mabusi alieleza kwamba DTB-Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo, wamekuwa wakilipa ada ya shule kwa watoto yatima watano kutoka kituo cha Kurasini katika shule ya sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha, pia wamukuwa wakichangia miche ya miti katika Wilaya ya Nyamagana -Mwanza, ikiwa na mtizamo wa kuboresha mazingira katika milima iliyoharibiwa na shuguli za kibinadamu.

Mkurugenzi wa fedha wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa tatu kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni baiskeli za wagonjwa ambapo pia walikabidhi vifaa tiba mbalimbali ikiwemo ni pamoja na magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam.

DTB-Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo) jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani City. Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dk. Amim Kilomoni akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka DTB-Tanzania

DTB-Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development – AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN)

 

Comments are closed.