The House of Favourite Newspapers
gunners X

Dtk. Mpango Kuongoza Mkutano wa Kimataifa wa Udhibiti Fedha Haramu

0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo anatarajia kuongoza Baraza la Mawaziri kutoka Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kitakachozungumza udhibiti utakatishaji fedha haramu.

Baraza hilo linatarajia kukutana Septemba 8, mwaka huu katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort, Visiwani Zanzibar. Aidha mkutano huo unatarajiiwa kutanguliwa na mkutano wa maofisa waandamizi, makatibu wakuu Septemba 2 hadi 6 mwaka huu kwenye hoteli hiyo.

Katika mkutano huo, pamoja na masuala mbalimbali yatakayojadiliwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatarajia kutumia fursa hiyo kuwasilisha taarifa ya hatua iliyofikia katika utekelezaji wa mpango wa chombo cha kimataifa kinachoshughulikia Uthibiti wa Utakatishaji wa Fedha Halamu ulioasisiwa mwaka 2009.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

Nyumba 900 Zabomolewa na Askari Kwenye Hifadhi ya Taifa ya Uzigua

Leave A Reply