The House of Favourite Newspapers

Dude alizwa kila kitu

0

dude1.jpgMwigizaji maarufu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Na Deogratius Mongela

YAMEMKUTA! Mwigizaji maarufu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amelizwa kila kitu kwenye gari lake baada ya wezi kuvunja kioo na kufanya uharibifu mkubwa kisha kutokomea na vitu hivyo.

Tukio hilo lililomchanganya Dude lilijiri nyumbani kwake, Kiwalani jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo jamaa hao waliruka fensi na kuvunja kioo cha nyuma kisha kutoa vitu muhimu kwenye gari hilo aina ya Toyota Mark II.

“Ukweli sasa hivi nikisikia kelele za mwizi hata niwe naendesha gari, nitapaki na kwenda kutoa kichapo.

Wamenirudisha nyuma sana. Yaani wamelisafisha kabisa gari langu kuanzia control box, redio, side mirror, betri ya gari, taa zote, spea tairi, jeki na vitu vingine,” alisema Dude akijiandaa kufungua jalada la kesi la kuwasaka wahusika.

Leave A Reply