The House of Favourite Newspapers

Dude: Rais Magufuli Kanyaga Twende

0

Stori: Gabriel Ng’osha 
HAPA mchezo! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amemtaka Rais John Pombe Magufuli kukanyaga spidi ya maendeleo kama alivyoonesha hivi karibu baada ya kuchaguliwa kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.

 Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda,Dude alisema D.k Magufuli anapaswa aendeleze na mshtukizo huo wa kutembelea kila wizara ili kuibua uozo wao.

“Kwa kweli kwa kuwashtukiza vile atawakamata wengi sana na kama akifanya kwa mwaka mzima, naamini sekta za serikali zitakuwa vizuri sana, watumishi watawahi kazini, uzembe utapungua na hata rushwa. Isiwe tu nguvu ya soda,alisema Dude.

Leave A Reply