The House of Favourite Newspapers

Dudubaya amepania kufanya kweli Maisha Basement

0

Dudubaya (2)
MWANAMUZIKI mkongwe, Dudubaya a.k.a Oil Chafu Au Mamba katika kukamilisha utambulisho wa kurejea kwake katika game, amepanga kufanya shoo kubwa wikiendi hii itakayokwenda kwa jina la Usiku wa Mamba.

Shoo hiyo itakayofanyika Jumapilli hii kwenye Ukumbi wa Maisha Basement, Dar es Salaam, Dudu amepanga kudondosha burudani ya kufa mtu kwa ajili ya mashabiki wake na wa muziki mzuri kwa ujumla.

mamba
Pia Dudu ameeleza kwamba shoo hiyo atasindikizwa na mkali Amini na wasanii wengine watakaokuwa ‘suprize’ kwa mashabiki watakaojitokeza katika usiku huo.

“Itakuwa shoo babkubwa yenye kiingilio cha Sh 10,000 na yatakayofanyika humo yatamkuna kila mmoja, kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kupigwa jukwaani kwa ngoma ya Kokoriko pamoja na shoo nyingine za wasanii wakali zitakazokuwa suprize kwa mashabiki wote,” alisema Dudu.

Leave A Reply