The House of Favourite Newspapers

DUDUBAYA JIPANGE UPYA ACHA KUTEGEMEA KIKI ZA ‘MASHOGA’

                    Godfrey Tumaini, KONKI! Konki! Konki master!

KONKI! Konki! Konki master!’ huu ndiyo msemo unao-trend kwa sasa mjini! Muasisi wake ni Godfrey Tumaini, wengi wanamfahamu kama Dudu Baya, yule msanii wa kitambo wa Bongo Fleva. Dudu Baya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na pengine kufutika katika vyombo vya habari, hivi karibuni ameibuka na mpya na kusababisha awe gumzo kubwa mpaka sasa.

 

Ishu ilianza kama masihara! Baada ya lile sakata la Amber Rutty ambalo nadhani wengi tunalifahamu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitangaza kuunda kamati maalum ya watu 17 kwa ajili ya kupambana na watu wanaofanya biashara chafu za ngono na mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume, yaani ushoga.

 

Makonda aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumtumia meseji zenye majina ya watu wanaojihusisha na biashara ya ngono pamoja na wanaume mashoga na hapo ndipo kizaazaa kilipoibuka. ‘Konki Master’ aliibuka kutoka kusikojulikana na kuja na orodha ya watangazaji watano aliodai eti ni mashoga. Orodha yake hiyo ilijaa majina ya watu wanaoheshimika katika jamii, kila mtu akashika mdomo kwa mshangao.

 

Hatujakaa sawa, Konki Master akaja na orodha nyingine ya  pili, akiwalenga waandishi wa habari na watangazaji na kama ilivyokuwa kwenye orodha yake ya kwanza, orodha ya pili pia ilikuwa imejaa majina ya watu maarufu, wanaoheshimika katika jamiii na wenye ushawishi.

 

Ilibidi baadaye jeshi la polisi liingilie kati kwa kumuita Dudubaya na kwenda kumhoji, baada ya hapo akasitisha zoezi la kutaja majina zaidi ya wale anaowatuhumu kwamba ni mashoga. Makonda alitaka atumiwe meseji za siri za majina ya wahusika, Dudu Baya akaamua kujirekodi video na kuwataja watu wenye majina makubwa, akiwatuhumu kwa skendo nzito ya ushoga!

 

Unaweza kujiuliza, kwa nini Dudu Baya amewalenga watu waliopo kwenye media? Inafahamika wazi kwamba waandishi wa habari na watangazaji pamoja na wasanii wanategemeana kwa karibu. Msanii anaweza kupata nafasi ya kuwika kwa urahisi kama ‘akibebwa’ na media, na msanii pia anaweza kushindwa ‘kung’ara’ hata kama ni mkali sana kama akibaniwa na media.

 

Kwa kipindi kirefu Dudu Baya amekuwa akijaribu kurudi tena kwenye gemu bila mafanikio, na mwenyewe amekuwa akiwalaumu watu wa media kwa kushindwa kumsapoti na badala yake kuwabeba wasanii wachanga wasio na uwezo wa kuimba.

 

Dudu Baya amesahau kama kila zama na kitabu chake, anataka media zimpe uzito sawa yeye na Aslay kwa mfano, hajui kama hivyo ni vizazi viwili tofauti  kabisa katika muziki. Ukitazama kila kinachoendelea kwa jicho la tatu, unaweza kupata picha kwamba alichokifanya Dudu Baya, kilikuwa katika sura mbili.

Sura ya kwanza, huenda alitaka kulipa kisasi cha watu wa media ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakimbania kama mwenyewe anavyodai. Amewahi kusikika akimtuhumu mtangazaji Hamis Mandi (B12) kwamba anambania kumpa nafasi kwenye shoo za Fiesta.

 

Sura ya pili, huenda ni kwamba ameamua kutembelea ‘upepo’ wa ishu ya mashoga kutafuta kiki! Na hapa amefanikiwa sana maana kila unakopita ni Konki! Konki! Konki Master! Sitaki kuzungumzia tuhuma ambazo zimeibuliwa dhidi yake pia, zikimhusisha na sakata hilo la ushoga!

 

Ninachotaka kuzungumza na wewe Dudu Baya, watu walikufahamu kwa sababu ya kazi, ulipata mashabiki kwa sababu ya kazi, nakiri kabisa kwamba ngoma zako kama Mwanangu Huna Nidhamu, Dege la Jeshi na nyinginezo, zilisaidia sana kuiweka Bongo Fleva katika ramani.

 

Kwa nini huelekezi nguvu kutoa ngoma kali kama wakongwe wenzako kina Profesa Jay ambao mpaka leo wanang’ara na badala yake unadandiadandia kiki zisizo na msingi na kuwaharibia wenzako ambao wametumia miaka mingi kuya-brand majina yao? Unajua ni kwa kiasi gani umesababisha madhara kwa hao uliowataja? Man up!

Comments are closed.