The House of Favourite Newspapers

Duh! Majimaji Kusajili Timu Nzima

0

KOCHA wa Majimaji FC ya Ruvuma, Kali Ongala ameibuka na kusema anahitaji kufanya usajili makini kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho kwa kuhakikisha kila nafasi inapata mtu mpya.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kally alisema wanahitaji kufanya maboresho makubwa katika kikosi chao katika msimu ujao wa ligi kuu kwa kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye viwango ili kuhakikisha wanakuwa na wachezaji wawili kila idara ili kuleta ushindani.

“Kwa sasa bado hatujaanza mchakato wa usajili japokuwa kuna baadhi ya wachezaji tunafanya nao mazungumzo kutoka timu mbalimbali kwa ajili ya kuwasajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi. “Nahitaji kusajili wachezaji 25 ambao watakuwa na viwango vinavyojitosheleza ili kuleta ushindani mkubwa kikosini,” alisema Kali.

KHADIJA MNGWAI | CHAMPIONI

Leave A Reply