The House of Favourite Newspapers

Duh! Yanga Kweli Wako Unga Dhidi ya DR Congo

TIMU ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imetajwa huku Yanga ikiwa na mchezaji mmoja tu kwenye kikosi hicho kinachoingia kambini leo Alhamisi kujiandaa na mchezo wa kufuzu Olimpiki Mchezo wa kwanza utachezwa Aprili 5, 2019 hapa nchini, kabla ya kurudiana ugenini Aprili 9, 2019.

 

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakar Shime ametaja kikosi cha wachezaji 27 huku wengi wakitoka JKT Queens.

 

Kikosi hicho ni: Fatuma Omar, Najiath Abbas, Maimuna Hamis, Fatuma Khatibu, Happyness Hezron, Stumai Abdallah, Anastazia Antony, Fatuma Bushir, Zena Khamis, Donisia Daniel, Asha Rashid, Fatuma Mustapha, (wote JKT Queens), Gelwa Lugomba, Asha Shaban na Irene Elias, (Kigoma Sisters).

 

Wengine ni Wema Richard, Tausi Abdalah (Mlandizi Queens), Enekia Yona (Alliance Queens), Fatuma Issa (Evergreen), Mwanahamis Omari, Amina Ally, Dotto Evalist na Amina Abdallah (wote Simba Queens). Pia wapo Aisha Khamis na Ester Mabanza (Alliance Queens), Grace Tony (Yanga Princess) na Niwael Makuruta (Marsh Academy).

Comments are closed.