DULLA MAKABILA KUMTAMBULISHA MREMBO WAKE DAR LIVE

MKALI wa Muziki wa singeli, Dulla Maka­bila amefunguka kuwa atamtambulisha mwa­namke wake wa sasa katika shoo ya Usiku wa Mwisho wa Ubishi itakayofanyika Aprili Mosi, (Sikukuu ya Pasaka) mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Za­khem, Dar.

 

Dulla, awali alikuwa akitoka na Husna Sajent kabla ya kumpiga chini na kumgeukia ‘rafiki’ yake Tiko Hassan ambapo kwenye shoo atakutana uso kwa uso na wakali wengine wa muziki huo ambao ni Man Fongo na Shollo Mwamba.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makabila alisema kuwa mbali na kujipanga kufanya shoo kubwa kwa ajili ya kuwafu­nika wapinzani wake, amepanga pia kumtambulisha mwanamke wake.

 

“Nimejipanga vya kutosha kwa kuwa na muda bado upo, naamini sitaweza kuwaangusha mashabiki wangu siku hiyo, kikubwa ni wao kujitokeza kwa wingi kuona nitakavyowaka­lisha wapinzani wangu kwa vitu nitakavyowaandalia.

“Kiukweli mashabiki wangu nimewaandalia vitu vingi sana lakini mmojawao safari hii ndani ya Dar Live nitawaletea mama yao wamuone kwa kumpandi­sha jukwaani, hiyo itakuwa ni fursa ny­ingine, kwa upande wa shoo nimeji­panga kwa kuwa naelewa watakuwa kina nani hivyo waje wenyewe kuona kitakachotokea,” alisema Makabila.

 

Kwa upande wa mratibu wa shoo hiyo na meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema mbali ya mchuano huo, ku­takuwa na ‘vita’ nyingine kadhaa za burudani.

KP Mjomba alionge­za kuwa kiingilio katika shoo hiyo ya aina yake kitakuwa ni buku saba yaani shilingi 7,000 huku michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo kuogelea ita­fanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi 12 jioni kwa shilingi 3,000.

 

 Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.


Loading...

Toa comment