The House of Favourite Newspapers

DULLAH MAKABILA ANASWA NA KIFAA KIPYA

Abdallah Ahmed ‘Dullah Makabila’ na Maiya Abdul

MSANII wa muziki wa Singeli, Abdallah Ahmed ‘Dullah Makabila’ hivi karibuni alinaswa na kifaa chake kipya anayejulikana kwa jina la Maiya Abdul ambapo walikuwa beneti kama kumbikumbi kila walipoenda.

Wawili hawa walinaswa ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo msanii wa filamu za maigizo nchini, Yvone Cherry ‘Monalisa’ alikuwa akizindua mpango wa kuwasaidia wasichana kufikia malengo yao kwenye tasnia ya filamu uitwao, Mona ACT.

Risasi Vibes lilipomuuliza Dulla kuhusiana na kugandana kwake na mrembo huyo alieleza kuwa ndiye mchumba wake anayetarajia kufunga naye ndoa muda wowote Mungu akipenda. “Huyu ni mchumba wangu anaitwa Maiya na hapa nimefika kwani tuna malengo mengi ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa Mungu akipenda,” alisema Dulla.

Comments are closed.