Dully afichua Harmonize alichofanya wimbo wa ‘Nikomeshe’ – Video

Msanii Dully Sykes alivyopokelewa leo katika ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori kwa ajili ya kutambulisha ngoma yake mpya aliyomshirikisha Harmonize, #NIKOMESHE.

MUDA mchache baada ya kutinga katika viunga vya Global Group, Sinza-Mori jijini Dar,  maalum kwa kutambulisha ujio wake mpya wa wimbo wa  Nikomeshe, mkongwe katika gemu la Bongo Fleva, Dully Sykes,  amefichua namna Harmonize alivyohusika katika ngoma hiyo.

…Akisaini katika kitabu cha wageni ofisini hapo.

Dully aliyasema hayo leo mchana mara baada ya kupokelewa kwa shangwe na umati wa wafanyakazi wa Global Group na kupelekwa  katika studio za +255 Global Radio.  Nyota huyo wa muziki wa vijana, alisema amekuwa karibu na Harmonize kwa ajili ya kufanya muziki wa kibiashara.

…Akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho.

“Katika wimbo wangu mpya na Harmonize wa Nikomeshe, ule kwanza sikutunga mimi, nilimwambia Harmonize anitengenezee wimbo wote,  mimi nilienda kuimba tu. Kwa hiyo ni ubunifu tu,” alisema Dully Sykes.

Meneja Vipindi wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka (kushoto) akimpeleka Dully kwenye idara mbalimbali kujionea kazi za uzalishaji (productions) katika ofisi hizo.

“Ukiona Harmonize ameweka katika ukurasa wake wa Youtube ile ni kazi, basi ujue ni yetu wote. Vidole viko vitano, unafikiri ukikata vinne kimoja kitakuwa na kazi gani?

…Akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Joseph Shaluwa.

 

“Shigongo wakati anafungua Global miaka ya 1999 kwanza kompyuta zenyewe zilikuwa hazipatikani na kulikuwa na ofisi ndogo tu ya watu wanne nakumbuka kwani nilikuwa mtu wa kwanza kufanya naye kazi.

 

 

…Akielekezwa jambo na Mhariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist.

“Leo hii nimeingia hapa (Global Group) nimeshangazwa kuona makampuni yameongezeka na kuwa mengi, watu wamekuwa wengi hata sikutegemea. 

“Kwa kipindi kile Shigongo angeamua kufanya kazi kama zamani na watu watatu tusingemsikia leo hii, tusingeisikia +255 Global Radio wala chochote cha Shigongo lakini kwa sababu alitafuta watu wa kufanya  nao kazi na kuwalipa, ndiyo maana yupo hapa leo hii,” alisema.

Dully ndani ya Studio za +255 Global Radio.

Dully alimaliza kwa kuwashukuru wafanyakazi wote wa Global Group na mashabiki kwa kuonyesha ushirikiano kila anapoachia wimbo mpya.

 

“Asanteni kwa sapoti yenu. Kufika na kupokelewa vizuri nimefurahi pia kwa kunipa nafasi kucheza ngoma zangu na pia mashabiki asanteni kwa kunikubali,  kila siku hamchoki, kwa kweli napendwa na watu hilo naomba niwashukuru.”

 

Kuyapata mahojiano kamili, tembelea Global TV Online katika Mtandao wa Youtube au ingia PlayStore (Bofya ===> rebrand.ly/255GlobalRadioApp)  katika simu yako na tafuta +255 Global Radio utapata fursa ya kusikiliza vipindi vyote vya kijanja mjini.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/ GPL / Picha na Richard Bukos

 

#EXCLUSIVE : DULLY SYKES Afunguka Kuhusu HARMONIZE, “Wanawake Wanazeesha sana..”

Loading...

Toa comment