The House of Favourite Newspapers

Dully Sykes Afunga Mjadala wa Ndoa

0

MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dullysykes’ amefunguka sababu ya kuwa bachela na kuufunga mjadala kuhusu suala la yeye kuoa.

Akizungumza na MIKITO NUSUNUSU, Dully ambaye kwa asasa anatamba na ngoma aliyofanya na Maua Sama inayokwenda kwa jina la Naanzaje, amesema suala la kuoa ni jambo dogo na watu wasipende kulichukulia kwa ukubwa.

“Unajua kuhusu suala la nitaoa lini huwa naulizwa sana eti nichukue mke kwa sababu nazeeka, naomba leo niwaambie watu kwamba suala la kuoa ni kitu kidogo sana wala wasipende kulichukulia kwa ukubwa kiasi hicho.

“Unajua hata kwa Mungu siyo ibada ya kusema kwamba eti mimi nitahukumiwa eti kwa sababu sijaoa, sitaki kuulizwa tena swali hili,” alisema Dully.

STORI: KHADIJA BAKARI, RISASI.

Leave A Reply